Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ureno Bi Trinidad Jimenez amemwambia rais Mahmoud Abbas anayeitembelea nchi hiyo kuwa Madrid inaunga mkono jitihada zote za Palestina kuunda taifa lake huru.
"Waziri alionesha kufurahishwa mno na hatua zilizofikiwa na nchi mbili hizi katika kuimarisha uhusiano wa kidugu katika kipindi cha miaka mingi iliyopita na pia kuunga mkono juhudi zote zinazolenga kuundwa kwa taifa huru la Palestina," taarifa ya Wizara ya Mambo ya Kigeni imesema.
Bi. Jimenez pia alimweleza Bwana Abbas kwamba juhudi za Palestina kuungwa mkono kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa ni haki kabisa na nchi yake itaiunga mkono Palestina katika suala hili.
Marekani imekuwa kimya katika kuunga mkono suala hili na imekuwa ikizitaka Israeli na Palestina kutochukua hatua itakayopelekea kuvurugika kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro huu.
No comments:
Post a Comment