RAMALLAH—Wafungwa wa Kipalestina waliomo katika magereza ya Israeli wapatao elfu saba hivi wameanza mgomo wao wa kutokula chakula kupinga mateso wayapatayo huko.
Tamko hilo limetolewa na vyama vitano vinavyowakilishwa huko magerezani.
Vyama hivyo ni: Hamas, Fatah, the Popular Front, Islamic Jihad, na Democratic Front.
Wamesema jambo hilo linatokana na msimamo wa Waziri Mkuu wa Israeli Bwana Benjamin Netanyahu kuweka sheria ngumu za magereza kwa wafungwa wa Kipalestina.
Wamesema jambo hilo linatokana na msimamo wa Waziri Mkuu wa Israeli Bwana Benjamin Netanyahu kuweka sheria ngumu za magereza kwa wafungwa wa Kipalestina.
Viongozi wote wa chama cha Hamas ambao ni wafungwa katika magereza ya Israeli wako chini ya uangalizi mkubwa na wamewekwa peke yao.
Wakati huo huo, ndugu na jamaa wa wafungwa hao wametanagaza maandamano makubwa kuunga mkono mgomo wa kutokula chakula kwa wafungwa hao.
Wamesema wataendelea na maandamano yao hadi hapo Israeli itakapo legeza msimamo wake wa kuwatesa wafungwa wa Kipalestina.
Unyama huo upigwe vitani haraka kunusuru maisha ya watoto na akina mama. Je, wanaharakati hamuyaoni hayo?
ReplyDelete