Sunday 10 July 2011

Ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015: Je, zitatekelezwa?


Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya kanda ya Ziwa - Nzega, Tabora
Mkoa wa Tanga kuwa jiji la viwanda - Tanga mjini
Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
Kulinda haki za walemavu - Makete
Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

No comments:

Post a Comment