TIGO KUWASHA
MOTO WA BURUDANI JIJINI DAR
Na Nasser
Kigwangallah, Dar es Salaam.
TIGO
itawasha moto wikiendi hii katika viwanja vya Coco Beach, jijini Dar es Salaam, ikisindikizwa na wasanii bora kabisa
nchini, watakaotoa burudani safi katika fukwe ya bahari ya Hindi.
Hayo
yalisemwa na Afisa Uhusiano Bi Alice Maro wakati akizungumza na waandidhi wa
habari kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Alisema maadhimisho
hayo ya siku mbili, ambayo ni ya mwanzo wa maonesho ya biashara yaitwayo ‘Sabasaba’ yatafanyika
kuanzia kesho Jumamosi Juni 30 na kesho kutwa Jumapili Julai 1, yataanza saa
tano kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.
Aliwataka
wasanii kutumia uwezo wao na vipaji vyao katika kuimba na kucheza sarakasi
katika mashindano ya Tigo ya kusaka vipaji vya chipukizi yaliyoandaliwa kwa wote
watakaohudhuria.
Au unaweza
kukaa na kuburudika pamoja na wanamuziki Mr Nice na H. Baba wakati
wakitumubuiza jukwaaani.
“Mwaka huu
tumeamua kuwaletea burudani nyingi na za kutosha ili kuweza kuwafariji wateja
wetu popote pale walipo, hivyo kufika kwao itakuwa faraja kubwa kwetu sisi,”
alisema Alice Maro, Afisa Uhusiano wa Tigo.
Aliongeza
kusema kuwa wanachotaka ni kwa wateja wao siyo kupata burudani tu, bali pia
waje wapate na kufurahia huduma zao zilizo bora kabisa na nafuu zilizoandaliwa
kwa ajili yao.
Alisema kilele
cha madhimisho hayo kitakuwa siku ya Jumapili kwa burudani kutoka kwa Juma
Nature, Roma Mkatoliki, Izzo B, Professor Jay, Mwasiti, Barnabas, Fid Q, Joe
Makini na burudani maalumukutoka kundi la wachekeshaji la “Ze Comedy.”
Hakutakuwa
na sababu ya kuondoka uwanjani jua likizama, kwani fainali za Euro mwaka 2012
zitakuwa zikianza wakati huo. Fainali hizo zitaoneshwa laivu katika skrini
kubwa kuanzia saa mbili usiku.
Kiingilio ni
bure kabisa na Tigo inawahamasisha wote kufika katika ufukwe wa Coco Beach ili
kusherehekea na kuukaribisha msimu huu wa Saba Saba.
KUHUSU TIGO
Tigo ni
mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania, ulioanza biashara mwaka
1994 na ni mtandao wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kuliko mitandao
mingine yote nchini unaotoa huduma katika mikoa 26, Tanzania bara na Visiwani.
Tigo ni sehemu
ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na inatoa huduma zake za intaneti
kwa gharama nafuu kabisa na ni mtandao wenye nguvu na kasi kubwa.
Mtandao wa intaneti
unapatikana maeneo mengi kwa urahisi zaidi kwa wateja wake wapaptao milioni 43
katika masoko 13 yanayoibukia barani Afrika na Amerika ya Kusini.
No comments:
Post a Comment