Monday 18 July 2011

MATATIZO YA U8MEME YATAKWISHA LINI TANZANIA? NI AIBU YA TAIFA

Mgao wa umeme unaoendelea Tanzania kwa sasa, ni ishara tosha kuwa serikali haijajipanga vizuri kulitatua suala hili kuanzia kiini chake hasa ni nini.
Wakati nchi hii ina kila sababu ya kujivuna kutokana na utajiri wake wa maliasili.
Je, tuseme ni maamuzi mabovu ya kiutendaji au kukosa kuwajibika ipasavyo kwa TANESCO na wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na Bwana William Ngeleja, waziri wa wizara hiyo? Bunge limeikataa bajeti ya wizara hiyo, serikali imetakiwa kuirekebisha na kuja na mikakati, baada ya wiki tatu kuanzia sasa. Hii haitoshi kumaliza mgao ambao umeathiri sekta zote za maisha ya wananchi na uchumi umeteketea kabisa. Kwa maoni yangu; serikali inatakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kwake kuwajibika ipasavyo.

No comments:

Post a Comment