Saturday 10 March 2012

Polisi wauaji watiwa ndani na kutimuliwa kazi Urambo- Tabora

Polisi wauaji wakiwa wameubeba mwili wa maraehemu Hasan Mgalula kwenye bajaj wakiupeleke kituoni. Huu ni unyama wa polisi hapa nchini kwetu

JESHI la Polisi nchini limewafukuza kazi askari wake wanne waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo raia mmoja mkazi wa mjini Urambo, Hassan Mgalula.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Rutta, alisema kuwa askari hao wamefukuzwa kazi kutokana na kujihusisha na tukio hilo baya.
Aliwataja askari hao ambao hivi sasa wanakabiliwa na tuhuma za mauaji kuwa ni Konstebo Aidano, Jonathan, Mohamed na Khakimu.
Kamanda Rutta alisema kuwa askari hao walioshikilwa kwa muda wa wiki moja, walikwenda kumkamata Hassan kwa tuhuma za kujeruhi na kutoa lugha chafu na huko waliamua kutumia nguvu iliyopita kiasi na kumpiga mtuhumiwa huyo ambaye alifariki.
Alisema kuwa watuhumiwa hao wanatarajia kufikishwa mahakamani mara moja ili kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.
Pichani police hao waliokuwa kuwa wamevaa kiraia wakiwa wamempakia marehem Hassan Mgalul kwenye bajaj huku wamemkanyaga kichwa! walipofika police walifungua file kuwa kapigwa na raia wenye hasira kali!

Kisa

inasemekana chanzo kilikuwa askari mmoja aliyekuwa kavaa kiraia kumgonga marehem kwa baiskeli, marehem alipohoji kwa nn kamgonga jamaa akaja juu, marehemakamshushia kipigo kikali, ndipo akafuata askari wenzake wakaja kumakamata jamaa na kumpa kichapo kabla ya kumtupia kwenye hilo bajaj la mizigo.

Eastern Africa Grain Council meeting in photo

Participants of a one day meeting on the effects of grain availability in Eastern Africa region, held recently at Peacock Hotel in Dar es Salaam.