Danny Mwakiteleko amefariki dunia Jumamosi Julai 23, 2011 baada ya ajali ya gari iliyotokea jijini Dar es Salaam, siku ya Jumatano usiku Julai 20, 2011, eneo la Tabata (ToT) na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala na baadaye Muhimbili.
Katika ajali hiyo, gari alilokuwa akiendesha Mwakiteleko liligongwa na lori lenye trela, ambalo lilitoweka bila kujulikana saa nne usiku.
Mwakiteleko alikuwa akitokea kazini New Habari Corporation, Sinza ambako alifanya kazi hadi saa tatu usiku.
Waandishi wa habari kadhaa wamekielezea kifo hicho kubwa ni pigo kubwa katika tasnia ya habari, hasa kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao marehemu enzi za uhai wake.
“Mwakiteleko alikuwa kamusi ya kitaaluma na kisima cha fikra,mfumbuzi na mbunifu wa kazi mbalimbali za kihabari na aliweza kufanya kazi zake na kuibua vipaji vya waandishi wengine,hakika wengi hawatakuja kumsahau,” anasema mmoja wa wana habari hao.
Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, amin...!
No comments:
Post a Comment