Monday, 11 July 2011

Sudan yagawanyika: Kaskazini ya Waislamu na Kusini ya Wakristo

Wakaazi wa Abyi
Rais wa Sudan Omar Al-Bashir ameelezea machungu yake baada ya taifa lake kugawanyika na kuwa nchi mbili. Hata hivyo amesema ilikuwa wazo njema katika kuafikisha amani.
Kiongozi huyo aidha ameonya kuzuka machafuko mapya dhidi ya eneo linalozozaniwa la Abyei.
Akizungumza na BBC siku moja baada ya uhuru wa Sudan Kusini ulioafikiwa kwa miongo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, Rais Bashir amesema ndoto yake imekuwa kudumisha taifa moja la Sudan.
Kiongozi huyo ameongeza ilikuwa muhimu matakwa ya raia wa Kusini kuheshimiwa ili kuepusha kurejelewa kwa mapigano.
Hata hivyo Bashir ametoa onyo kali kwa Sudan Kusini.
Amesema kuna hatari ya kuzuka mapigano upya ikiwa maafikiano dhidi ya maeneo yanayozozaniwa hususan Abyei hayataheshimiwa.
Amesisitiza Abyei ni himaya ya utawala wa Khartoum na itakuwa jimbo la Kusini pale raia wafugaji wataridhia kuwa chini ya Juba kupitia kura ijayo ya maoni, matukio ambayo huenda yasinafinikiwe.

No comments:

Post a Comment