Wednesday 6 July 2011

Meli ya Kifaransa yaondoka Ugiriki na kuelelekea huko Gaza



BRUSSELS--- Meli moja ya Kifaransa yenye msaada wa kibinadamu imeondoka jana huko Ugiriki na kuelekea Gaza, wakati meli nyingine kwenye msafara huo zikiwa bado zimezuiliwa katika bandari mbalimbali za Ugiriki.

Lengo la msafara wa meli hizo ni kuvunja vizuizi vilivyowekwa na Israeli kwa wananchi wa Gaza ambao wanataabika kutokana na kukosa huduma muhimu kama vile chakula, madawa, elimu na afya bora.

Meli hiyo ya Kifaransa iitwayo “Dignity” iliondoka jana katika bandari ya Ufaransa ya Corsica ili kuvunja vizuizi hivyo vya Gaza.

Meli hiyo hivi sasa inaelea katika bahari upande wa maji ya kimataifa, Bwana Rami Abdo, msemaji na mratibu wa msafara huo amesema.

Meli hiyo, amabyo ina wanaharakati sita, ina lengo la kupamabana na Uzayuni na wafuasi wao wanaowaunga mkono.

 Maafisa wa utawala wa Ugiriki wameamaua kuzuia meli sita za msaada kuondoka katika bandari zake na kwenda Gaza kama zilivyopangwa.Kitendo hicho kimewaudhi wanaharakati hao ambao wamedhamiria kwenda Gaza kwa namna yeyote ile.

.............

1 comment: