UKOSEFU wa sera nzuri za uchumi hasa katika masuala ya kilimo na chakula imeelezwa ndio chanzo cha matatizo mengi ikiwemo kusababisha njaa na ukame unaopelekea wanawake na watoto wengi Afrika kuathirika.
Akifungua tamasha la wiki ya jinsia
lenye kauli mbiu Jinsia,demokrasia na maendeleo"Ardhi nguvu kazi na maisha endelevu",Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Ghana Profesa Dzotdzi Tsikata alisema matatizo mengi yanayotokana na ukosefu wa chakula ,ukame,madini,nishati maji na mazingira husababishwa na sera mbovu zilizopo katika sekta ya chakula na kilimo jambo linalosababisha wanawake na watoto walio pembezoni kuwa katika mazingira magumu.
"Tatizo hili linaweza kuwa na kihistoria kutokana na mifumo iliyokuwa wakati wa ukoloni na hata baada ya uhuru na mifumo mibivu ya kiuchumi ulio katika nchi nyingi za Afrika jambo linalosababisha rasilimali nyingi katika sekta za utalii,madini na ardhi kuchukuliwa na wawekezaji wa kimataifa"alisema Profesa Tsikata na kufafanua kuwa,
Kutokana na rasilimali hizo kuchukuliwa na walowezi na wawekezaji ta kimataifa wasiojali wananchi wa kawaida, kundi kubwa la wananchi ambao ni wengi wao ni wanawake hubaki katika mazingira magumu kutokana na kukosa ardhi watakazozitumia kufanya uzalishaji wa chakula na kufanya shughuli zingine za kuchumi zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi na kuepukana na majanga hayo.
Tsikata alisema ardhi ni rasilimali muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi au binadamu yoyote lakini kutokana na mifumo ya unyonyaji,ukandamizaji, na uchumi kwa wawekezaji wakubwa kumesababisha utabaka.
"Hivyi basi ili kuondokana na matatizo hayo ni vizuri nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kuwa na sheria na sera nzuri zinazowaruhusu wanawake kumiliki ardhi kama ilivyo Kenya".
alifafanua kuwa sera zilizotungwa miaka ya themanini kwame haziwezi kuleta mabadiliko katika ulimwengu uliopo sasa kutokana na mifumo ya kiuchumi na kisiasa ilivyobadilika.
"Kamwe sera na sheria zilizotungwa miaka ya themanini haiwezi kuleta mabadiliko ya mapinduzi ya kilimo na viwanda yaliyodhamiriwa sasa badala yake itazidi kudumaza harakati za kuleta mabadiliko"alisema Tsikata.
Alizitaja baadhi ya nchi za zilizoingia katika matatizo na migogoro ya ardhi kutokna na kutokuwepo kwa demokrasia na
sera nzuri ni pamoja na Afrika kusini,Guinea Bisau,Swaziland,Ghana na Malawi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Tanzania ,Mary Rusimbi alisema kuwa tamasha hili limekuja wakati muafaka nchini tukaribia kusheherekea miaka hamsini ya uhuru japokuwa tunakumbwa na changamoto kadhaa katika kujileta mabadiliko.
“Moja ya mambo tutakayopenda yafanyiwe kazi katika miak 50 ya uhuru ni pamoja na mabadiliko ya katiba yatakayoleta mabadiliko ya kimapinduzi katika masuala ya jinsia.”alisema Rusimbi.
Alifafanua kuwa "hili na tamasha linahudhuriwa na watu zaidi 2000 litatoa fusra kwa wanaharakati kujadili na kubadilishana mawazo, kufanya tathmini ya mafanikio na changamoto zilizopo kwa ajili ya kutafuta mbinu kukabili matatizo hayo ili kuleta mabadiliko kwa jamii kwa mtazamo wa wanawake kimapinduzi'.
No comments:
Post a Comment