MSAFARA wa kwanza kabisa katika historoa ya bara la Afrika, ukiwa na shehena ya vyakula na msaada mwingine umeanza safari yake kuelekea Gaza.
Msafara huo, ukiwa na wanaharakati ishirini na moja na magari zaidi ya kumi, umebeba aina mbalimbali ya misaada inayohitajika huko Gaza, eneo la Palestina ambalo limewekewa vizuizi na utawala wa Israeli kwa muda mrefu sasa.
Misaada hiyo ni madawa, maziwa ya unga, majenereta, vifaa vya ujenzi, na mahitaji mengine muhimu kwa wananchi waishio huko.
Msafara huo umeanza ulianza juzi huko Durban, nchini Afrika ya Kusini na unatarajiwa kufika Gaza mwishoni mwa mwezi ujao, yaani Julai.
“Leo hii tumesimama hapa, bila ya masharti yeyote kuunga mkono juhudi za kimataifa dhidi ya wananchi wa Palestina ambao wanateseka. Mungu awabariki mkiwa safarini kuelekea katika nchi ambayo mutawafikia Wapalestina,” alisema Bwana Michael Abrahams katika ofisi ya Meya wa jiji la Durban.
Magari yote yaliyomo katika msafara huo yatatolewa bure kama msaada kwa halmashauri za miji ya Palestina.
Waandaji wa msafara huo wamesema lengo lao siyo kupeleka msaada tu huko gaza, bali pia kuhamasisha kote Afrika ambako msafara huo utapita, juu ya madhila yawapatayo wananchi wa Palestina huko Gaza kutokana na unyama wa Israeli.
Wananchi wapatao milioni moja na nusu hivi wanaishi kwa taabu kutokana na kukosa huduma muhimu za hospitali, elimu na mambo mengine ya kila siku.
Hilo ni jukumu la kila mtu
ReplyDelete