Thursday, 4 August 2011

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Haruna Masebu akifafanua jambo juu ya mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini.
 
SIKU moja tu baada ya EWURA,kutangaza bei mpya za mafuta hapa nchini wafanyabiashara wamegoma kushusha bei.
Jana na leo jijini Dar es salaam, vituo vingi vya mafuta bado vimefungwa, kwa kile wafanyabiashara hao kukiita 'bei mbaya-watapata hasara.'
Hapa ndipo mimi ninapojiuliza iweje wafanyabiashara wachache waigomee serikali?
Na je, kwa mtindo huu, nchi inapelekwa wapi"
Serikali yenyewe itashidwa kufanya kazi kwa kukosa hii nishati.
Ipo hatari kubwa nchi hii kuongozwa na wafanya biashara, walanguzi na mafisadi.
Mfano wa hivi karibuni tu serikali ilitoa tamko la kushusha bei ya sukari na unga, hadi sasa bado bei juu, jambo ambalo linathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya mwananchi wa kawaida.
Jana bungeni kumeibuka kashfa nyingine ya kifisadi: Pamoja na maagizo kuoka kwa Waziri Mkuu kukataza kuuzwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) bado liliuzwa na wajanja; mafisadi.

No comments:

Post a Comment