Sunday, 28 August 2011

Kutoka Hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda (26.08.2011) 'Makampuni yanayoogoza kwa kulipa kodi Tanzania'

Mr Mizengo Pinda, the primer minister of Tanzania

Among the leading taxpayers companies in the country, only one mining company (the smallest ino Resolute T), and only one telecom company.
Banks lead, household names like MeTL, Bakhresa, IPP, VodaCom, Barrick, AngloGold Ashanti are not seen in the list, why? No body knows for sure.
One can conclude that, Tanzania Breweries Limited (TBL) is the most profitable company in Tanzania while National Micro-finance Bank (NMB0 is said to be the most profitable Bank in the country.
Mheshimiwa Spika,
1---Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:
 i.  dTanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);
 ii.  National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);
 iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);
 iv.  National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);
 v.   CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);
 vi.  Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);
 vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);
 viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);
 ix.   Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);
 x.    Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);
xi.   Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);
xii.  Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);
 xiii. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);
 xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na
 xv.  Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).
 
2. --- Napenda kutoa rai kwa Makampuni yote Nchini kuiga mfano huu mzuri. 
Wito wangu kwa makampuni, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo na wananchi wote ni kuongeza juhudi katika kufanya biashara zao ili zizalishe kwa wingi na kupata faida kubwa zaidi. Faida kubwa itachangia katika kuongeza mapato ya serikali kwa njia ya kodi na hivyo kusaidia kukuza uchumi, kuongeza pato la taifa na la mwananchi mmoja mmoja na kuondoa umaskini. Niwadhihirishieni kwamba, serikali inatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya nchi yetu na itahakikisha inaongeza juhudi zake za kuweka mazingira wezeshi kwa makampuni hayo kufanya shughuli zao vizuri ili kuwezesha kulipa kodi kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment