Wednesday, 6 July 2011

POSHO ZA WABUNGE ZIFUTWE: NI MZIGO KWA WANANCHI MASKINI



















POSHO ZA WABUNGE ZIFUTWE: NI MZIGO KWA WANANCHI MASKINI





UFAFANUZI uliotolewa na waziri mkuu bungeni hivi karibuni ni kioja kitupu na ni kupotosha ukweli wa mambo.

Hivi ni kweli kuwa wabunge wanalipwa ili nao wakawape wapira kura wao fedha, watawapa wangapi?

Nadhani waziri mkuu hakusema ukweli, kwani ulimi uliteleza.

Hawa jamaa akina Kabwe Zitto siyo kwamba wanataka posho zote zifutwe hapana, ni posho moja tu; tena ndogo sana ambayo ni posho ya kukaa kwenye kiti tu(sitting allowance) ambayo ni shilingi 70,000/- kwa siku kwa kila mbunge na kila mkurugenzi, mkuu wa idara, katibu mkuu na maofisa wengine wanapokaa kwenye viti vyao kwa ajili ya kikao cha kikazi ambacho ni sehemu yao ya kazi za kawaida.

Ukweli wa mchanganuo na mishahara ya wabunge na posho zao ni kama ifuatavyo:

Tangu Novemba, 2010 hadi Novemba, 2015 bunge lingine litakapochaguliwa; kila mbunge atakuwa akilipwamshahara wa mwezi 7,500,000/-; posho ya diesel lita 700 kwa mwezi ili aweze kutembelea jimbo lake vizuri na kila lita imepigiwa mahesabu ya 2,500/-

Jumla ni 1,750,000/- kwa mwezi; posho ya dereva kila mwezi 400,000/-

Posho ya katibu wa mbunge kila mwezi 400,000/-; posho ya matengenezo ya gari la mbunge ni 1,000,000/- kwa kila mwezi na posho ya vikao vya kamati, bunge, semina na vikao vingine kwa mwezi ni wastani wa siku 15 kila mwezi, kila siku ni 80,000 (posho ya kujikimu) na 70,000/- (posho ya kukaa kitini (sitting allowance), jumla posho ya vikao, semina nk ni 150,000/- kwa siku ambayo kwa siku 15 ni Shilingi 2,250,000/-.

Ukijumlisha mshahara na marupurupu mengine, yaani mshahara na posho zote hizo maana wengi wao hata zile za madereva na makatibu wao huzichukua wao wenyewe; utakuta mbunge wa Tanzania anakunja milioni 13 kwa mwezi mmoja.

Ukiondoa kodi kwenye mshahara ya 525,000/- anabakiwa na takribani 12,775,000/- anazoipelekea familia yake nyumbani kwake.

Hapo umeshaondoa fursa zingine ama kusafiri nje ya nchi ambapo hulipwa 800,000/- kwa siku.

Posho ambayo CHADEMA wanaikataa ni ile posho ya kukaa tu kwenye kiti 70,000/- kwa siku.

Kwa maana hiyo, posho zenye mantiki wanazikubali; posho hiyo ikiondolewa inapunguza malipo kwa mbunge kwa mwezi kwa 1,050,000/- tu; yaani badala ya kulipwa 12,775,000/-, posho hiyo ikiondoloewa kila mbunge atalipwa 11,725,000/- kwa mwezi.

Faida kwa nchi inayoweza kupatikana kutokana na punguzo hilo ni kuokoa 4,309,200,000/- kwa mwaka, ambazo zinaweza kuingizwa kwenye bajeti ya maendeleo.

Fedha hizo zinaweza kuchimba visima vya maji 287 vyenye uwezo wa kuhudumia watu wapatao 100,000 kwa mwaka.

Kwa miaka mitano ina maana watu 500,000 watafaidika na punguzo hilo.

Je, Watanzania wengine mna maoni gani? Ukiondoa posho zote za kukaa tu kwenye kiti serikalini na mashirika ya umma (total sitting allowances), unaweza kuokoa zaidi ya 90,000,000,000/-!

Wanawake wanajidhalilisha ovyo, je tunakwenda wapi?



Discpline at school: Can we cope this situation in Korea?

The death of print has long been on the minds of journalists, writers, bloggers, etc.
For those of us who grew up reading our books on paper, asking for magazine subscriptions, and watching our dads read the paper (on paper) at the breakfast table, it’s hard to imagine a world without a book case, and the handful of novels we never got around to picking up yet.
In South Korea, there seems to be much less fear over a paperless world, as the country has promised to replace all the paper in its schools by 2015.

Tuesday, 5 July 2011

The legacy of Mwalimu Julius K. Nyerere in Tanzania: How do you remember him?




The lateMwalimu
Julius K. Nyerere, how Tanzanians remember him?

Nyumba ya Mzee Nelson Mandela iliyoko Soweto, jijini Johannesburg





Nyumba ya mkongwe wa siasa za Afrika ya Kusini, Mzee Nelson Madiba Mandela iliyoko katika kitongoji cha Soweto jijini Johannesburg ambako alikuwa akiishi kabla ya kukamatwa na utawala wa makaburu kwa tuhuma za uchochezi na kutiwa gerezani huko Rhodes Island. Nyumba hiyo hivi sasa haikaliwi na mtu yeyote, imefanywa kuwa ni makumbusho; kuenzi enzi za mkongwe huyo. Picha: Na Nasser Kigwangallah, aliyekuwa Johannesburg hivi karibuni.

Mbunge wa Tabora mjini, Bwana Aden Ismail Rage: We are watching you, sir!

Aden Ismail Rage, honourable MP for Tabora constituency (a town which has been neglected for quite sometime now), vowed to uplift the lot of local people in Tabora township and its adjacent; who are poor in everything. The question here is: will he actually manage to do just that?

Wabunge wetu Tabora: Je, ninyi ni wapambanaji ambao mtatuletea maendeleo mkoani kwetu au ninyi ni ;opportunistst' tu?







Wabunge kutoka mkoa wa Tabora: 1. Dk. Athumani Rashid Mfutakamba- Igalula, 2. Dk. Hamisi A. Kigwangallah (a.k.a Said Nassor Kigwangallah), 3. Profesa Juma Athumani Kapuya- Urambo Magharibi, 4. Samwel John Sitta- Urambo Mashariki, 5. Rostam Abdulrasul Aziz- Igunga, 6.Saidi Juma Nkuba- Sikonge

Monday, 4 July 2011

Anti-Gaza blocade activists intend to sail to Gaza for sending humanitarian relief goods

Israel said it was bracing itself for a "provocation fly-in" by pro-Palestinian activists who were planning to board flights to Ben-Gurion airport in Tel Aviv.
"The planned provocation and its participants will be dealt with according to Israeli and international law...the event continues attempts to breach Israel's borders by sea, land and air," a written statement from Prime Minister Benjamin Netanyahu said.
Pro-Palestinian websites have called in recent weeks on activists to fly to Israel on July 8 to protest policy toward the Palestinians, with the aim of coinciding with arrival of the flotilla, floundering in recent days.

Unyama wa Israeli huko Gaza


RAMALLAH—Wafungwa wa Kipalestina waliomo katika magereza ya Israeli wapatao elfu saba hivi wameanza mgomo wao wa kutokula chakula kupinga mateso wayapatayo huko.

Tamko hilo limetolewa na vyama vitano vinavyowakilishwa huko magerezani.

Vyama hivyo ni: Hamas, Fatah, the Popular Front, Islamic Jihad, na Democratic Front.

Wamesema jambo hilo linatokana na msimamo wa Waziri Mkuu wa Israeli Bwana Benjamin Netanyahu kuweka sheria ngumu za magereza kwa wafungwa wa Kipalestina.

Viongozi wote wa chama cha Hamas ambao ni wafungwa katika magereza ya Israeli wako chini ya uangalizi mkubwa na wamewekwa peke yao.
Wakati huo huo, ndugu na jamaa wa wafungwa hao wametanagaza maandamano makubwa kuunga mkono mgomo wa kutokula chakula kwa wafungwa hao.
Wamesema wataendelea na maandamano yao hadi hapo Israeli itakapo legeza msimamo wake wa kuwatesa wafungwa wa Kipalestina.

TGNP kutoa mafunzo kwa wanaharakati mikoa mitano nchini


 
Kuanzia tarehe 28 Juni hadi 1 Julai 2011, kwa muda wa siku nne, Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP)  utasambaza wafanyakazi wake katika kanda tano nchini  kukutana na wanaharakati wa ngazi ya jamii  kwaajili ya warsha ya kujengeana uwezo na nguvu za pamoja katika  kujenga tapo la mabadiliko katika jamii, ambalo litachangia kuwepo kwa jamii yenye mabadiliko, yenye kutambua na kuthamini masuala ya jinsia, demokrasia, haki za binadamu na haki za kijamii.

Mafunzo haya yatalenga kujenga nguvu za pamoja katika kuendeleza kampeni ya haki ya uchumi katika ngazi ya jamii kwa kuongeza  uelewa wa maana ya ‘Haki ya Uchumi: Rasilimali Ziwanufaishe Wanawake Walioko Pembezoni’ kwa mtazamo wao wenyewe kwa kuzingatia mjadala mpana wa uundaji wa Katiba mpya.

 Mikoa ambayo imepata fursa hiyo kwa kipindi hiki ni Kanda ya  Kaskazini Mkoa wa Kilimanjaro, Kanda ya Mashariki Mkoa wa Morogoro,  Kanda ya Kati ni Mkoa wa  Dodoma, Kanda  ya Ziwa ni Mkoa wa Shinyanga na nyanda za Juu Kusini ni mkoa wa Ruvuma. Baada ya warsha za wanaharakati kutafuatiwa na mafunzo ya waandishi wa habari  namna ya kuandika habari za kijinsia  katika mikoa ya Ruvuma na Shinyanga.

 Katika mafunzo hayo, kutakuwa na timu ya watu wawili kutoka TGNP  na mmoja kutoka katika kanda husika. Zoezi hili muhimu litaendeshwa kwa mbinu za kiraghbishi  ili kuwapa wananchi nafasi ya kujadiliana zaidi, kuibua changamoto na fursa za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni  walizonazo na jinsi wanavyoshirikiana kuzitatua na kama hazitatuliwi ni hatua gani wanachukua kuzitatua. Mwishowe wataweka mikakati madhubuti kwa hatua zaidi za utekelezaji na  tathimini.

Pamoja na hayo, TGNP itatumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika mchakato mzima wa kuandika katiba mpya  na nafasi ya mwanamke katika mchakato huu. Kadhalika TGNP itaelezea kwa kina juu ya Tamasha kubwa la Jinsia litakalofanyika jijini Dar es salaam tarehe 13-16, Septemba, 2011,  namna watakavyoweza kushiriki.



Infrastructure improvement