The Tigo Tanzania General Manager Mr Diego Gutierrez delivering his speech at the launch of Tigo-Pesa Border Transfer between Tanzania and Rwanda at a ceremony held at Serena Hotel in Dar es Salaam today
The Rwandan High Commissioner His Excellency Dr. Ben Rugangazi making his inaugural speech at the launch of Tigo-Pesa cross country money transfer at a ceremony held at Serena Hotel in Dar es Salaam today
Dar
es Salaam, Tanzania and Kigali, Rwanda: 24 Februari, 2014
– TIGO, kampuni ya mawasiliano ya kimataifa inayomilikiwa na Millicom (Stockholmsbörsen: MIC) ambayo ni kampuni
inayoongoza katika nchi 13 barani Afrika na Amerika Kusini, imekuwa kampuni ya
kwanza duniani kuanzisha huduma ya kutuma na kupokea pesa baina ya nchi mbili
tofauti ambazo ni Tanzania na Rwanda.
Huduma
hii mpya ilizinduliwa katika tafrija mbili tofauti kwa wakati mmoja ambazo zilifanyika
katika miji ya Dar es Salaam na Kigali ambapo Balozi wa Rwanda nchini Tanzania
Dr. Ben Rugangaza na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Bw. Francis Mwaipaja ndio
walikuwa wa kwanza kufanya miamala ya kutuma na kupokea pesa kupitia njia ya simu
kati ya nchi hizo mbili.
Huduma
hii inatoa fursa kwa watumiaji wa Tigo nchini Tanzania kutuma pesa kwa njia ya
simu kwa kutumia huda ya Tigo Pesa kwenda kwa watumiaji wa Tigo nchini Rwanda,
na kinyume chake. Huduma hiyo inaweza ikabadilisha fedha za kigeni moja kwa
moja, ambapo pesa inayotumwa kwa shilingi za kitanzania au francs za Rwanda
zinaweza zikabidilishwa kuwa fedha za nchi zinakopokelewa.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, aina hii ya huduma ni ya
kwanza duniani kwa kuwa na uwezo wa kubadilisha fedha za kigeni kutoka kwa
mtumaji hadi kwa mpokeaji.
Fedha ikishapokelewa kwenye simu, mteja
anaweza kuitumia kulipia huduma zote zinazopatikana kwenye Tigo Pesa au Tigo
Cash iliyopo Rwanda. Hii inajumuisha kuongeza salio, kulipia bili ya maji, TV
pamoja na usafiri, kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti za benki, kutoa fedha
kutoka kwa wakala yeyote nchini pamoja na kutuma kwa urahisi fedha kwa
watumiaji wengine wa Tigo Pesa.
Kutuma fedha kutoka Tigo Pesa (Tanzania)
kwenda kwa watumiaji wa Tigo Cash (Rwanda), mteja anachotakiwa kufanya nia
kupiga nambari *150*90#, huku wale walioko Rwanda wakipiga nambari *200*7#.
Huduma hii inaweza ikatumika kutoka kwenye simu aina yeyote iliyounganishwa na
laini ya Tigo. Wateja wa nchi husika watapokea fedha zao pale pale wanapotumiwa
na kupokea katika aina ya fedha ya nchi husika.
Kujisajili kwenye huduma ya Tigo Pesa au Tigo
Cash, wanachotakiwa kufanya wateja ni kutembelea wakala yeyote nchini Tanzania
au Rwanda. Kujisajili ni bure. Kinachohitajika ni kitambulisho cha mhusika.
Kwa mujibu wa Gutierrez, “Huduma hii mpya
itaokoa muda mwingi wa wateja pamoja na fedha zao. Watumaji wa fedha kimataifa wamekuwa
wakienda sehemu za kubadilishia fedha za kigeni kuweza kubadilisha Francs za
Rwanda kuwa dola kasha kutuma hizo dola kupitia kwa mawakala wengine wa fedha.
Hivi sasa wanaweza wakatuma pesa kupitia simu zao.”
Gutierrez aliendelea: “Tunafurahi kuwapa wateja
wetu nyenzo za kufanya miamala kwa wana Afrika mashariki wenzao. Tunashukuru
kwamba kutokana na teknolojia yetu ya kisasa, wananchi wa Rwanda wanaweza
kutuma pesa kwa familia, marafiki, pamoja na wafanyabiashara wenzao walioko nchini
kwao.”
Tongai Maramba, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Rwanda naye
alisema: “Tumefurahi kuanza kuwapa wateja wetu wa Tigo Cash uwezo wa kutuma
fedha kimataifa kupitia simu zao. Pia ni jambo zuri zaidi kwamba wateja wetu
wamerahisishiwa kwa kuweza kupokea moja kwa moja katika Francs za Rwanda kwa
sababu kampuni nyingi za kutuma na kupokea fedha huwa wanatumia dola. Huduma
hii haimpi wasi wasi wowote mteja kuanza kutafuta sehemu ya kubadilishia fedha.”
Murenzi Abdallah, msafirishaji anayefanya kazi
katika kampuni moja ya usafirishaji kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali na Goma
alisema: “Nimefurahishwa sana na uwezo tuliopewa wa kutuma na kupokea pesa kwa
njia ya simu nikiwa nchini Tanzania. Maisha yangu yatarahisishwa kwa namna ya
kukamilisha kulipia ushuru mbali mbali mpakani pamoja na mahitaji mengine
nikiwa katika safari zangu ndefu.”
Millicom inatoa huduma za kutuma na kupokea fedha
nchini Tanzania, Ghana, Rwanda, DRC, Chad, Bolivia,
Colombia, El Salvador, Guatemala, Honduras, Senegal na Paraguay, pia ina mpango
wa kuzidi kupanua wigo wake katika nchi zingine katika siku za usoni.
Huduma
hii mpya ina manufaa makubwa kwa biashara zinazofanyika kati ya nchi hizi
mbili, familia zinazokaa katika nchi hizi kama wageni, waendesha malori, wanaosafirisha
na kununua.
No comments:
Post a Comment